Jumatano, 5 Oktoba 2016

http://www.stinhanzi.com/2016/10/haya-hapa-magazeti-ya-leo-alhamisoktoba.html

Fafanua fonolojia ya Kiswahili





CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHA DAR ES SALAAM  (DUCE)
KITIVO CHA HUMANITIA NA SAYANSI JAMII
IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU

KOZI: FONOLOJIA YA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI: KI 208
KIONGOZI WA SEMINA: MICHAEL A MASHAURI
CHUMBA CHA SEMINA: LR/A
SIKU YA SEMINA: JUMATANO
MUDA WA SEMINA: SAA 5:00 -5:55 ASUBUHI
WASHIRIKI
NA
JINA KAMILI
NAMBA
PROGRAMU
SAHIHI

1

2014-04-0
BAED


2

2014-04-
BAED


3
MLIMAKIFI HANZISTIN M
2014-04-05700
BAED


4
MAGUKU DENES MAGOMBA
2014-04-05195
BAED


5
KIDAVA SAYUNI N
2014-04-05428
BAED



SWALI LA 2:
Fafanua fonolojia ya lugha ya Kiswahili. 
MPANGO KAZI
UTANGULIZI
Maana ya fonolojia
Maana ya fonimu
KIINI
Vipengele mbalimbali vya fonolojia

HITIMISHO

MAREJELEO


Kwa mujibu wa TUKI (1990) Anasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushugulikia uchambuzi wa sauti zinazotumika katika mfumo fulani. Mgullu (1999)  Akimnukuu Hartman 1972 anasema kwamba fonolojia ni mtalaa wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani na uamilifu wao ndani wa mfumo lugha inayohusika. Massamba na wenzake (2004) Wanasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu  linaljishughulisha na uchambuzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za binadamu. Kinachosemwa hapa ni kwamba fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahsusi. Hivyo kipashio cha kifonolojia ni fonimu. Fonimu kwa mujibu wa Daniel Jones (1967) Wanasema kuwa ni kipashio kidogo zaidi cha mfumo wa sauti ambacho hutumika kubainisha maana za maneno mawili ya lugha moja. Massamba (2004) anasema fonimu  ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi kuweza kukitofautisha na a vipande vingine vya aina yake. Massamba na wenzake (2004) Wanasema fonimu ni kitamkwa kilichobainifu katika lugha fulani maalumu. Hivyo tunaweza kusema kuwa fonimu kipashio kidogo ch kifonolojia kinachoweza kuweza kubadili maana ya neno katika lugha fulani (mahususi). 
Mfano           pata                  bata
                      Kura                kula
        Oa                    ua
Hivyo basi fonolojia inajihusisha na vipengele vikuu viwili ambavyo ni vipande sauti na vipengele arudhi. Vipande sauti ni kipengele ambacho kinashughulikia uchunguzi wa vipande vyenyewe, wanaisimu katika aina hii hubainisha vipande sauti bainifu katika lugha kama vile alofoni na fonimu pia kueleza fonimu hizo jinsi zinavyoweza kuathiriana katika maneno mbalimbali. Vipande sauti hivyo ni irabu na konsonanti. Irabu kwa mujibu wa Massamba na Wenzake (2004) anasema irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi na kuwepo kizuizi chochote katika mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywa  na chemba ya pua. Hii ina maana kuwa irabu zote ni ghuna. Hivyo lugha ya Kiswahili inazo jumla ya irabu tano (5) ambazo ni i,e,a,o na u. na vipo vigezo vikuu viatu vinavyo tuongoza kubaini/ kuainisha irabu kama vile mahali pa kutamkia, mwinuko wa ulimi, na hali ya midomo.
Mahali pa kutamkia. Irabu huweza kutamkwa katika sehemu tatu za ulimi. Sehemu 
               MBELE             KATI                    NYUMA
  /i/                        /u/
/ԑ/ /ᴐ/

/a/
Mwinuko wa ulimi. Katika sifa hii kinachoangliwa ni jinsi ulimi unavyoinuka yaani kama irabu ya chini irabu inapotamkwa ulimi upo chini. Irabu ya kati ulimi unakuwa kati na irabu a juu ulimi unakuwa juu.

                               /i/                                      /u/        JUU
                                                                                                                                                                                     
/ԑ/  /ᴐ/       KATI
/a/ CHINI






Hali ya midomo. Hapa sifa hii inaangaliwa kama midomo imeunda umbo la mviringo au haijaunda yaani ipo mtandazo. Hivyo tuna sifa viringe na si viringe. Tafiti zinaonesha kuwa irabu za mbele hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa, lakini irabu za nyuma hutamkwa midomo ikiwa mviringo.
irabu
Sifa kutokana na hali ya midomo

i, ԑ
Irabu si viringe

ᴐ,u
Irabu viringo


Konsonanti kwa mujibu wa Massamba na wenzake(2004) wanasema ni sauti ambazo katika utamkaji wake mkondo hewa huzuiwa kutoka mapafuni kupitia katika chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Uzuiwaji wa mkondo hewa unaweza kuwa wa kubana au kuachiwa taratibu kama kutamka sauti /ch/. Wikipedia.org/wiki/Matumizi ya lugha. Anasema kuwa konsonanti zinapotamkwa hewa huzuiliwa na ala za matamshi. Kuna vigezo vikuu viwili vinavyotumika kuainisha konsonanti za lugha ya Kiswahili ambazo ni 
Mahali pa kutamkia, hapa kinachoangaliwa ni konsonantiimetamkwa wapi kama ni konsonanti ya meno, ufizi, midomo. Konsonanti za midomo ni [m], [p],[b]. konsonanti za midomo meno kam vile [f] na [v]. konsonanti za meno hizi hutamkwa kwa kutumia meno ya juu na ncha ya ulimi sauti kama [θ] na [ð], konsonanti za ufizi, hizi hutamkwa kwa kutumia ufizi mfano wake ni sauti kama vile  [n], [t], [d], [s]. konsonanti za kaakaa gumu, hizi ni konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake hutegemea sehemu ya juu ya chemba ya kinywa kama vile [ʧ] na [j], konsonanti za kaakaa laini, hutamkwa katika sehemu inayoanza na mara baada ya kaakaa gumu [k], [g], [ŋ]. Konsonanti za glota, hizi ni aina ya konsonanti ambazo hutamkiwa katika koromeo mfano [h]
Hali ya mkondo hewa, kinachoangaliwa hapa ni namna ya utamkaji yaani hli ya mkondo hewa kuzuiwa moja kwa moja na kuachiwa ghafla, kuzuiwa kidogo na kuachiwa ghafla, hewa hewa kutoka kwa kukwama kwama, aina hizo ni pamoja na: vipasuo hizi ni aina ya konsonanti ambazo wakati wa utamkajihewa kutoka mapafuni hubanwa na kuachiwa ghafla. Kama vile [b], [k], [g].  vipasuo kwamizi, hewa huzuiwa na kuachiwa polepole na kupita kwa kukwama kwama kama vile [ʧ], [j], vikwamizi hizi ni konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake hewa huzuiwa na kuachiwa kupita katika nafasi ndogo ya ala za sauti zilizo karibiana na hivyo hewa kupita kwa kukwaruza mfano [θ], [f], [v] na [z]
Hali ya nyuzi sauti, kinachoangaliwa hapa ni kama nyuzi sauti zinatikiswa na hivyo kurindima na kutoa mghuno au hazirindimi na hivyo hazitoi mghuno. Ghuna nyuzi sauti hurindima na kutoa mghuno mfano [b], [g], [n], [ŋ]. Konsonanti si ghuna ni zile ambazo nyuzi sauti hazirindimi kama vile [f], [θ] [h], [s].
Sifa bainifu za fonimu, hizi ni kama zifuatazo;
Usilabi, sifa hii huainisha fonimu yenye sifa ya kuwa na usilabi na ambaz hazina sifa hiyo ya lugha yakiswahili sanifu. Irabu zote pamoja na nazali katika mazingira maalum huwa na sifa a usilabi na zilizobaki yaani konsonanti zote na nazali huwa hazina usilabi [+sil].
Mfano              mtoto                $m $to $to $
Sifa ya mghuno yaani mtetemo wa nyuzi sauti. Sifa hii huainisha fonimu za Kiswahili zile zenye mghuno na zisizo na mghuno. Irabu zote ni ghuna, nazali na viyeyusho.
Mfano               [a], [i], [m], [y]
Sifa ya mwachano taratibu taratibu [±tar] sifa hii ni sauti inayotolewa wakati hewa ikiachiwa taratibu.
Mfano      ch       [ʧ] 
Unazali, nazali zote zina sifa ya unazali [+naz] vitamkwa vinavyobaki havina sifa hiyo.
Mfano:                 [m], [n], [ŋ].
Ukontinuanti, [±kont] sifa hutumika kubainisha sauti ambazo zimetamkwa wakati mkondo hewa ukiwa wazi bila kuzuiliwa mahali popote.
Mfano:      irabu zote na nazali.
Umadende, [±mad] sifa hii hutumkika kwa ala sogezi kugonga gonga kwa haraka kwenye ufizi.
Mfano:           [r]  rudi
Sifa za mahali pa matamshi 
Uanteria. Sifa hii inahusu vitamkwa kuanzia kwenye ufizi kwenda mbele yaani ufizi [d], meno [f], midomo [b] na [m].
Umeno, sifa hii inahusu vitamkwa ambavyo hutamkwa wakati ulimi ukiwa katikati ya meno.
Mfano:     [ð], [Ɵ]
Dhambi,  Thamani,  
Kanuni za michakato ya kifonolojia.
Uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho (w) na (y) irabu yeyote ya juu ( iwe /i/ na /u/)  ikifuatana na irabu isiyo fanana nayo katika neno irabu hiyo hubadilika na kuwa kiyeyusho.
Mfano:   umbo la ndani           umbo la nje
   /mu+isho/                [mwi:sho]
   /Mu+anzo/                [mwa:nzo]
   /mu+embe/               [mwe:mbe]
Hapa tunaona wazi kwambi katika lugha ya Kiswahili, irabu ya juu nyuma /u/ hubadilika na kuwa kiyeyusho/w/ kutokana na kufuatiwa na irabu ambayo haifanani nayo mchakato huu unaweza kuoneshwa na sheria/ kanuni ifuatayo.
/u/                          [w] I ≠ u
Pia katika kuunda kwa kiyeyusho /j/ mfano ni kama ifuatavyo,
Umbo la ndani                 umbo la nje
                    /Mi+ezi/                         /mje:zi/
                    /vi+ungu/                       vju:ungu/
Katika mifano hii huona wazi kwamba irabu ya juu mbele imebadilika na kuwa kiyeyusho /j/ kutokana na kufuatiwa na irabu ambayohaifanani nayo mchakato huu unaweza kuoneshwa na 
/i/                          [j]/                 I ≠ i
Ukakaishaji, kwa mujibu wa Massamba (ametajwa) anasema ukakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu ni sifa zisizo za kaakaa gumuzinapobadilika na kuwa za kaakaa gumu. Lugha ya Kiswahili ina fonimu mbili za kaakaa gumu ambazo ni /j/ na  /ʧ/ maelezo hayo yanaweza kuthibitishwa na mifano kutoka katika lugha ya Kiswahili.
Umbo la ndani                            umbo la nje
/ki+ angu/           [cha:ngu]
/ki+ombo/ [cho:mbo]
Mchakato huu unaweza kuoneshwa kanuni ya kifonolojia ifuatayo.
/k/                      [ʧ]/                     i + I ≠ /i/
Hata hivyo kanuni inaweza vigairi kama inavyothibitika katika miufano ifuatayo. 
              Umbo la ndani                            umbo la nje
/ki+ oo/   [choo]
/ki+ atu/   [chatu]
Udondoshaji wa irabu, ni mchakato wa kifonolojia ambapo irabu inadondoshwa wakati ambapo jambo moja mojawapo kati yafuatayo yanapotokea. Wakati ambapo irabu inafuatiwa na konsonanti ya kweli na wakati ambapo irabu zinafuatana
Mfano:         Umbo la ndani                            umbo la nje
/mu+zigo/                                    [mzigo]
/mu+ dogo/      [mdogo]
Katika data hii tunaona kwamba irabu /u/ inadondoshwa inapofatiwa na konsonanti ya kweli. Mchakato huu unaweza kubainishwa na kanuni ifuatayo.
U                [Ɵ]/ /m/           K (halisi)
Pia irabu inaweza kudondoshwa ikifuatana na irabu nyingine kama inavyoo    nekana katika mifano ifuatavyo;
Umbo la ndani                            umbo la nje
/wa+limu/                                      [walimu]
/Wa+angu/                [wangu]
Mchakato huu unaweza kuwakilishwa  kwa kanuni ifuatayo 
          /a/            [Ɵ]               ⁺ [a] 
Yaani irabu /a/ inadondoshwa katika mazingira ambapo inafuatiwa na irabu inayofanana katika mpaka wa mofimu 
     Usimilisho pamwe wa nazali; katika mkururo huu wa nazali na konsonati, nazali huathiriwa na konsonati inayofuata. Usimilisho huu hutegemea mahali ambapo konsonati hiyo hutamkiwa. Hapa nazali hupewa umbo jumuishi /N/.
       Mfano ;            Umbo la ndani                            umbo la nje  
                            /n+buzi/                                            [mbuzi]
Hivyo mchakato huu unaweza oneshwa kwa kutumia kanuni hii ifuatayo 
               /N/                  [m]/                    /b/
Fonimu jumuishi (N) inajitokeza kama [m] katika mzingira ya kufuatiwa na [b]
        Kuimarika kwa fonimu;pale ambapo fonimu hafifu hubadilika nakuwa  na kuywa yenye nguvu ,kuimarika kwa fonimu ni kule kuongezeka kwa nguvu za misuli na msukumo wa mkondo hewa wakati wa utamkaji fonimu husika
    Mfano    Umbo la ndani                            umbo la nje
                     /n/+refu/                             [ ndefu]
                 /n+limi/                                  [ndimi]
Kwa kutumia mifano hiyo tunaona wazi /r/na /l/ zinabadilika na nakuwa /d/ pale zinapotanguliwa na nazali ya ufizi /n/ ,mchakato huwa kama ifuatavyo ;
               r   
            l                        [d]    N
            Kudhohofika kwa fonimu; hapa fonimu iliyokuwa ikitamkwa kwa nguvu  hutumia  sauti nguvu kidogo, 
       Mfano;    Umbo la ndani                            umbo la nje
                       /mpendi/                                         [mpenzi]
                     / Mpiki/                                           [mpishi]
Hapa tunaona wazi kuwa /d/ hubadilika na kuwa  [z] na /k / kuwa/  /pale zikifuatiwa na irabu i yaunominishaji mchakato huo ni huu ;
                 d                            z                         I     ya unominishaji.
              k
     
Pia folojia hushughulikia vipengele arudhi katika lugha vipengele arudhi ni vipengele vya fonolojia vinavyoshughulikia sifa zaidi  ya vipande sauti. Vipengele arudhi ni kama vile 
mkazo, ni utamkaji wa nguvu zaidi katika sehemu ya neon au fungu la maneno, utamkaji huu hufanywa katika silabi na hutokea katika silabi ya pili kutoka mwisho katika lugha ya Kiswahili.
Mfano:   mwali’mu
Hayu’po
Mzu’ri
Kiimbo, kwa mujibu wa Massamba na wenzake (2004) ni kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti. Katika lugha ya Kiswahili, kiimbo hutusaidia kuelewa au kubaini lengo la msemaji kama vile;
 kutoa maelezo (-) mfano.  Atafika leo mchana
 kuuliza swali (/)  mfano.    Kwanini? 
 kutoa amri (/) mfano.    Ondokeni hapa. 
Lafudhi, ni sifa yakimasikizi ya matamshi ya mtu binafsi ambayo humpa msemaji utambulisho fulaniwa kijamii au wa kieneo. Katika lugha ya Kiswahili, lafudhi hutufanya tuweze kutofautisha kati ya watu wa pwani na bara. Hii inatokana na athari ya lugha za mwanzo yaani lugha mama, watu wa bara Kiswahili ni lugha yao ya pili wakatti watu wa pwani ni lugha yao ya kwanza.
Kiswahili sanifu.                   Kiswahili cha kusini
Mtoto anaumwa.                  Ntoto anaumwa.
Toni, Mgullu (1999) Anasema toni ni kiwango cha kidatu pamoja na mabadiliko yake ambayo hutokea wakati mtu anpotamka silabi au maneno. Katika lugha zenye toni mabadiliko yake hubadili maana za maneno. Ila katika lugha ya Kiswahili hatuna toni.
Kidatu ni kiwango cha juu, cha kati,au cha chini katika usemaji pia kidatu ni kile kiwango cha sauti kisikikacho yaani katika usemaji mtu anaweza kuongea kwa sauti ya juu yaani kidatu cha juu, kwa sauti ya kati yaani kidatu cha kati, kidatu cha chini yaani sauti ya chini.na mawimbi sauti huwa yanabaki yaleyale.
Hivyo basi 

MAREJELEO
http://sw.m.wikipedia.org/wiki/Matumizi ya Lugha.
Massamba na Wenzake (2004), Fonolojia ya Kiswahili Sanifu FOKISA, TUKI: Dar es Salaam.
Mgullu, R.S (1999), Mtaala wa Isimu, Fonetiki na Fonolojia ya Kiswahili, Nairobi: longhorn publishers.
Palome, E (1967), A Handbook of Swahili Language
TUKI, (1990) Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha, TUKI: Dar es Salaam.

UMUHIMU WA ZAWADI KATIKA MAHUSIANO. 

1. ZAWADI ZINABORESHA MAPENZI: Umuhimu wakwanza wa Zawadi katika mapenzi ni kuboresha mapenzi. Fahamu kuwa unapompa mpenzi wako zawadi utamfanya ajihisi kama niwapekee kwako hivyo atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na ataamini kama kweli upo karibu yake na unamjali hivyo hatashindwa kulipa mazuri kwako kwa kukuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako kwani atakua anajua kuwa wewe unamjali na unamuonesha upendo sasa kwanini nayeye asikujali?! Hivyo zawadi yako itakuwa ni njia moja wapo ya kuboresha penzi lako kwa umpendae.
2. ZAWADI ZINAJENGA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI: Umuhimu wa pili wa zawadi katika mapenzi ni kujenga taswira ya kumbukumbu kwa mpenzi wako, faham kuwa unapompa mpenzi wako zawadi inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana nawewe kwake kunatofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila azionapo zawadi zako.
Mpenzi msomaji wa ukurasa huu napenda nikushauri juu ya zawadi unazotakiwa kumpa mpenzi wako jitahidi pindi unapohitaji kumnunulia mpenzi wako zawadi tafuta zawadi ambayo itadumu kwa mpenzi wako kama vile nguo, card, maua n.k. Isiwe zawadi ya muda mfupi isiyotunzika kwa mfano unaweza kumpa mpenzi wako hela ila jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara ya mapenzi. KUMBUKA: simaanishi kuwa usimpe mpenzi wako hela hapana ila inabidi ufaham kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.
Itaendelea......

Kwa maoni na ushauri tuwasiliane 0758273121   

Jumanne, 4 Oktoba 2016

tafsiri na ukalimani

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM (DUCE) KITIVO CHA HUMANTIA NA SAYANSI YA JAMII IDARA YA LUGHA NA ISIMU JINA LA KOZI: TAFSIRI NA UKALIMANI MSIMBO WA KOZI: KI311 MKUFUNZI WA KOZI: CHIPALO AMANI AINA YA KAZI: SEMINA SIKU YA SEMINA: JUMATATU, SAA: 4:00 ASUBUHI WAHUSIKA NA JINA NAMBA ZA USAJILI PROGRAMU SAINI 1 KOMBA FREDRICK 2014-04-05576 BAED 2 MLIMAKIFI HANZISTIN2014-04-05700BAED 3 NDUNGURU STELA 2014-04-05648 BAED 4 NYIWALA JANE 2014-04-07968 BAED 5 KASSANGA PUDENSIANA2014-04-05404BAED 6 KIDAVA SAYUNI 2014-04-05428 BAED 7 PASIANI EDINESTA 2014-04-05206 BAED 8 MPANGO KAZI UTANGULIZI Maana ya Semantiki kwa mujibu wa walaalamu. Maana ya Fahiwa, Utajo na Urejeleo. KIINI Kufanana na kutofautiana kwa “utajo”, “Urejeleo” na “Fahiwa”. Jinsi dhana hizi zinavyofanikisha au kukwamisha kupata maana katika lugha HITIMISHO MAREJELEO Baadhi ya wataalamu wamejaribu kutoa fasili ya Semantiki kwa kuzingatia vipengele mbalimbali kama ifuatavyo; Lyons (1968) anasema “Semantiki ni taaluma ya maana”. Udhaifu wa fasili hii ni kwamba mtaalamu huyu hajaelezakuwa maana hiyo imejikita katika kipengele gani, je kipengele cha maneno au sentensi. Masamba (2004:75) anasema “Semantiki ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchambuzi na uchunguzi wa maana ya maneno na tungo katika lugha” Kwa ujmula, Semantiki ni taaluma inayojushughulisha na uchambuzi na uchunguzi wa maneno au viambajengo vya maneno au leksimu katika lugha. Taaluma hii inadhana za msingi zinazotumika kurejelea maana katika lugha. Zifuatazo ni dhana hizo ambazo ni “Utajo”, “Urejeleo” na “Fahiwa’; Utajo, Lyons (1977)anasema “Ni uhusiano kati ya leksimu na seti ya vitu ambavyo vinarejelewa na leksimu hiyo”. Dhana hii inatokana na neno taja au kutaja. Uhusiano huo hurejelea vitu kwa majumui. Mfano kiyambo pombe hurejelea pombe za aina zote duniani, mfano watu wakiwa baa mmoja akitaja pombe ataulizwa pombe gani kwani neno hilo linataja aina zote za pombe ulimwaenguni. Pia neno chakula hurejelea hurejelea vakula vyote kama ugali, wali, pilau na viazi. Urejeleo,Yule (1996:17) “Ni kitendo cha mzungumzaji au mwandishi kutumia alama za kileksimu kumuwezesha msomaji au msikilizaji kutambua kitu kinachosemwa”. Kwa ujumla, urejeleo ni uhusiano baina viambo vya lugha na na viwakilishi vyake duniani, wakati maalumu wa semo na mkutadha, urejeleo huweza kutaja kitu mahususi, Mfano kama hapa chini; Chakula ugali, wali, pilau na viazi Pombe bia, mbege, chibuku na ulanzi Nyama ya kuku, ya mbuzi ya bata na nyama ng’ombe Katika mifano hii tunaona kuwa maneno yaliyokiolezewa wino ni maneno mahususi yanayorejelewa na leksimu kuu. Mfano mzungumzaji akitaka kutaja kitu lazima ataje kitu mahususi. Fahiwa, Matinde (2012:261) anasema “Ni dhana ya leksimu inayowakilishwa na neno tofauti na kirejelewa chenyewe”. Hivyo tunaweza kusema fahiwa ni mahusiano yaliyopo baina ya kiyambo kimoja na viambo vingine katika lugha, mahusiano hayo huitwa mahusiano ya kifahiwa. Ifuatayo ni mifano ya mahusiano ya kifahiwa; Usinonimia, ni hali inayojitokeza au iliypo pale ambapo maneno mawili au zaidi yenye maumbo tofauti na maana moja au inayokaribiana. Maneno hayo huitwa sinonimia au viswe. Mfano: fedha, hela na pesa. Mjinga, bwege na mpumbavu Jembe, mchizi, mshikaji na msela. Mifano hii inaonesha maumbo tofauti yenye maana zinazo karibiana. Uantonimia au unyume, ni uhusiano wa kimaana baina ya maneno mawili ambapo maana ya neno moja ni kinyume cha nenolingine, uhusiano wa maneno hayo huitwa antonimia. Mfano nyuma inakuwa mbele, mwanamke inakuwa mwanaume, kubwa inakuwa ndogo. Umeronimia, ni uhusiaono ulipo baina ya leksimu inayotaja sehemu ya kitu na leksimu inayotaja kitu kizima, mfano mwili sehemu zake ni kichwa, mihuu, mikono, mabega na tumbo pia ukitaja kichwa kuna macho. Masikio, mdomo na nywele.Hiyo ni mifano kadhaa inayoonesha mahusiano ya kifahiwa katika luhga. Ufuatao ni ufanano uliopo baina ya “Utajo”, “Urejeleo” na “Fahiwa”; Zote ni dhana za muhimu zinazodokeza maana kwa undani zaidi. Mfano ukitaja rangi na baadae ukataja aina mahususi kama njano, bluu na nyekundu basi inamsaidia mtu kupata maana mahususi, pia fahiwa husaidia kupata maana kwa kutumia neno kulingana na mahitaji yake, mfano katika unyume. Pia zote husaidia katika ujifunzaji wa lugha, mfano wakati wa kumfundisha mtoto mdogo tunataja neno pamoja na kirejeleo chake kama ukisema kiti basi unamuonesha kiti hicho, pia katika maneno kama kisu, jembe na embe ukimtajia basi unamuonesha virejelewa vyake. Zifuatazo ni tofauti zilizopo katika dhana hizo; Utajo hurejelea vitu kwa ujumla au majumuhi, mfano nyumba au chakula bila kutaja aina zake lakini urejeleo hutaja vitu mahususi, mfano katika chakula urejeleo hutaja aina mahususi ya chakula lama vile ugali, wali na viazi, pia katika pombe basi hutaja aina mahususi ya pombe. Fahiwa huweza kuibua utata katika maneno lakini urejeleo hauibui utata katika maneno, katika fahiwa uhomonimia huweza kuibua utata kama msemaji au mwandishi hatazingatia mkutadha,mfano katika maneno haya; Kaa –mdudu Kuketi Moto Ganda la kibiriti Panda – weka mbegu aridhini kwea Mgawnyo wa njia mbili Zifuatazo ni namna dhana hizi zinavyoweza kufanikisha maana katika lugha; Dhana ya utajo hufanikisha maana katika lugha kwa kutaja vitu au maneno kimajumui, kupitia dhana hii humsaidia mtumiaji wa lugha kupata maana kwa ujumla. Mfano kujua matunda kama neno majumuhi baadae atajua aina zake. Urejeleo humsaidia mtumiaji wa lugha kupata maana mahususi kwani hutaja neno na kurejelea kitu mahususi katka mkutadha huo. Mfano ukitaja meza lazima utataja aina mahususi kama meza ya chuma, meza ya mviringo, meza ya mbao. Fahiwa inafanikisha kupata maana za maneno yenye maumbo tofauti tofauti yenye uhusiano kimatumizi lakini katka mkutadha fulani au maalumu na pia maana ya neno katka seti kuu. Mfano; pesa, hela na fedha. Tundu, shimo na tobo. Fahiwa humsaidsia mtumiaji wa lugha kupanua maana au kukuza lugha, kwa kupitia uantonimia, mtu apatao dhana au maana ya neno panga ni rahisi kwake kujua maana ya neno pangua kwa kuwa maneno haya yana maana kinzani. Zifuatazo ni namna dhana hizi zinavyoweza kukwamisha maana katika lugha; Katika urejeleo kuna maneno mengine hayana virejeleo maalumu mfano maneno kama viunganishi, vivumishi nivigumu kupata vireleleo nyake hivyo basi yakisimama peke ni vigumu kupata maana. Pia kuna dhana kama Mungu, malaika na shetani ni vigumu kupata virejeleo vyake. Baadhi ya dhana huweza kusababisha utata katika lugha, mfano utajo huweza kuleta utata kwa sababu kitajwa chake si mahususi. Kama mtu akitaja meza bila kutaja aina muahususi ya meza hiyo itamuwia vigumu msikilizaji au msomaji kupata maana kamili. Hata fahiwa husababisha utata hasa pale mtu anapotumia neno lenye maana zaidi ya moja kama vile shuka, lia na panda, maneno haya huleta utata katika kupata maana. Kwa ujumla, kiatika Semantiki dhana hizi hutumika katika lugha ili kupata maana, pia dhana hizi hutegemeana kulingana na matumizi yake katika lugha, kwa kutumia nadharia mbalimbali za maana na aina za maana hujumuisha katika upatikanaji wa maana katika lugha. MAREJELEO Lyons, J (1968). Introduction to Theoretical Linguistic. New York: Cambridge University Press. Liyons, J (1977). Semantics. Great Brutain: Cambridge UNiveristy Press Masamba, P. B. D (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI Yule, G (1996). Pragmatics. New York: Oxford University Press.

Matokeo kidato Cha pilibofya hapa

 KUTAZAMA BOFYA HAPA <https://matokeo.necta.go.tz/ftna2020/ftna.htm>