Jumatano, 4 Januari 2017
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHA DAR ES SALAAM (DUCE)
KITIVO CHA HUMANITIA NA SAYANSI JAMII
IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU
KOZI: FONOLOJIA YA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI: KI 310
CHUMBA CHA SEMINA: LR/D
SIKU YA SEMINA: JUMANNE
MUDA WA SEMINA: SAA 10:00 -10:55 ASUBUHI
WASHIRIKI
NA JINA KAMILI NAMBA PROGRAMU
1 NYAKIHANGA STELLA 2014-04-08100 BAED
2 KILUMILE LUCIA 2014-04-05356 BAED
3 MLIMAKIFI HANZISTIN M 2014-04-05700 BAED
4 NDOPWELY PUDENCIANA 2014-04-05223 BAED
5 MWAKASEGE FATUMA 2014-04-05737 BAED
6 NICOLA JOHN G 2014-04-05989 BAED
7 MSILA AGATHA 2014-04-08048 BAED
8 MROPE SHUWEA 2014-04-05176 BAED
9 AHMAD AHMAD YUSUF 2014-04-07497 BAED
10 ISMAIL MUSSA 2014-04-07911 BAED
SWALI LA 9: Tumia mifano ya Kiswahili kufafanua dhana ya uelekezi wa vitenzi.
MPANGO KAZI
UTANGULIZI
Maana ya uelekezi
Maana ya vitenzi
KIINI
Aina za vitenzi:
Vitenzi elekezi
Vitenzi si elekezi
Darajia za vielekezi:
Utendwa
utendewa
HITIMISHO
MAREJELEO
Dhana ya uelekezi imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo:
Massamba (2004) anafafanua uelekezi kuwa ni uhusiano uliopo baina ya kitenzi na vijenzi vingine vya kimuundo wa sentensi vinavyohusiana nacho.
Habwe na Karanja (2004) wanaeleza kuwa uelekezi ni hali ya kitenzi kuruka mipaka na kuathiri maneno mengine ya sentensi. Maneno hayo yanayoathiriwa huwa ni yambwa au yambiwa.
Kihore (2001) anaona uelekezi kuwa ni uwezo wa kitenzi kinachoundwa na mzizi fulani kuchukuana na yambwa katika muundo wa sentensi.
Wren na Martin (2007) wanafasili kuwa uelekezi ni hali ya kitenzi kuashiria tendo linalofanywa na mtenda au kiima likiwa na yambwa.
Mkude (1995) anafafanua uelekezi kuwa ni uwezo wa kitenzi kujitosheleza kimuundo yaani iwapo kitenzi kinahitaji kujalizwa na kipashio kingine ili kifanye kazi kikamilifu.
Kwa ujumla, uelekezi ni dhana inayohusu hali ya kitenzi kubeba au kutobeba yambwa au yambiwa. Ni dhahiri kuwa dhana ya uelekezi ina uhusiano wa moja kwa moja na na kikundi tenzi. Hivyo ni vyema kukielewa vizuri kitenzi cha Kiswahili.
Kitenzi ni kategoria ambayo ni muhimili wa kikundi tenzi cha Kiswahili, ni nguzo au kielelezo muhimu cha sifa bainifu za lugha ya Kiswahili. Kitenzi ni neon linaloeleza jambo lililotendwa au linalotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo. Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti. Pamoja na kudokeza uelekezi, kitenzi cha Kiswahili hudokeza pia mambo mbalimbali kama vile kauli, njeo, pamoja na hali. Hivyo kuna aina mbalimbali za vitenzi ambavyo ni
Kwa kutumia kigezo cha uelekezi, Aristotle anagawa vitenzi vya Kiswahili katika makundi mawili ambayo ni Vitenzi si elekezi na Vitenzi elekezi.
Vitenzi si elekezi, Hivi ni aina ya vitenzi ambavyo havihitaji kujalizwa na yambwa au yambiwa (kiathirika na mnufaikaji/ mfaidikaji) ili kukamilisha maana katika sentensi kama inavyooneshwa katika mifano ifuatayo:
Nyani amekufa.
Ndege ameruka.
Fatuma ameolewa.
Giza limeingia.
Rose anacheka.
Jonas anakoroma.
Meza imevunjika.
Jua linawaka.
Flora amenuna.
Vitenzi katika sentensi hapo juu hazihitaji yambwa kwa kuwa vitenzi vyenyewe vilivyotumika vinajitosheleza kimawasiliano (kimaana). Hatuwezi kwa mfano katika sentensi hizo tukabaki tunajiuliza maswali ambayo ni lazima yajibiwe. Mifano zaidi ya vitenzi hivyo ni duwaa, kua, zaa, ngaa, imba, kaa. Dhana ya kitenzi si elekezi hujitokeza katika kitenzi ambacho hakiruhusu kuchukua nomino nyingine. Hapa kitenzi kinawekewa hali ya utendeka inayojidhihirisha katika umbo la –k na –ik.
Mfano: kikombe kimevunjika.
Maji yamechemka.
Vitenzi elekezi, hivi ni vitenzi ambavyo huhitaji kujalizwa na nomino moja au mbili. Kwa maneno mengine, vitenzi elekezi ni vile vyenye uwezo wa kungoeka/ kubeba yambwa na/ au yambiwa. Vitenzi elekezi vyaweza kuwa elekezi kwa hulka yake au kwa kunyambuliwa. Unyambulishaji unaweza kuathiri kitenzi sielekezi kuwa elekezi kwa kukiongezea, kupunguza au kudhibiti vihusika vinavyoambatana nacho. Vitenzi elekezi vimegawanyika katika makundi mawili nayo ni vitenzi elekezi mara moja na vitenzi elekezi mara dufu.
Vitenzi elekezi mara moja, hivi ni vitenzi elekezi vyenye kubeba yambwa moja tu. Kama inavyojidhihirisha kwenye mifano ifuatayo:
Mkude amejenga nyumba.
Habibu amenunua gari.
Kalou ameleta machungwa.
Shangazi anapika ugali.
Vitenzi vilivyomo katika sentesi hizo hapo juu zinahitajia yambwa moja ili kujikamilisha kimawasiliano. Mifano ya vitenzi vyenye hulka sawa na hivyo ni pamoja na tenda, iba, osha, pika, suka, soma nk. Vitenzi vyote hivyo vina tabia zinazofanana.
Vitenzi elekezi mara dufu, hivi ni vile vitenzi ambavyo vinahitaji kujalizwa kwa yambwa mbili ili viweze kujikamilisha kisarufi. Mifano ifuatayo inadhihirisha ukweli huu:
Mwalimu amempa Asha ujumbe wake.
Meya alimkabidhi katibu mali zake.
James alimpiga mpenzi wake kofi.
Mwalimu alimpa mwanafunzi kalamu.
Vitenzi vyote katika sentensi hizo vinahitajia kufuatwa na yambwa zaidi ya moja. Vitenzi elekezi mara dufu siyo vingi sana katika lugha ya Kiswahili ukilinganisha na vitenzi elekezi mara moja.
Hivyo kuna darajia za uelekezi kama ifuatavyo, uelekezi uko katika darajia mbili ambazo ni utendwa yaani kiathirika na utendewa yaani mfaidikaji/ mnufaikaji.
mfano :
Kaka alimchumia baba yake maua.
Mama alimuandikia baba barua.
Mwajuma anampikia mmewe ugali.
Nomino zilizokolezwa ni yambwa tendewa ambazo zinanufaika na tendo lenyewe na zile zisizokolezwa ni yambwa tendwa yaani zinaathirika na tendo moja kwa moja.
Ikiwa sentensi ina yambwa tendwa na tendewa, basi kitenzi chake hubeba kiambishi cha yambwa tendewa. Iwapo sentensi ina yambwa tendwa tu, basi kitenzi chake pia chaweza kubeba kiambishi yambwa. Kanuni hii inazua utata kuwa ni katika mazingira gani kiambishi yambwa chaweza kuwepo katika kitenzi na kutokuwepo katika kitenzi kama inavyojidhihirisha katika mifano ifuatayo:
Huseni anaikata nyama.
Edward anamkatia nyama mama.
Salma anamjengea baba nyumba.
Fatuma alimnunulia shangazi gari.
Shangazi anampikia mgeni ugali.
Ukilinganisha mifano yote ya vitenzi vyenye uwezo wa kubeba yambwa utaona kuwa tofauti ya kungoeka au kutongoeka yambwa moja au mbili inathiri pia uwezo wa kitenzi kubeba au kutobeba kiambishi yambwa.
Hivyo kwa kuhitimisha tunaweza kueleza kuwa japokuwa kuna vitenzi elekezi na vitenzi si elekezi katika dhana hii ya ulekezi wa vitenzi, bado aina kuu za vitenzi inabaki palepale ambapo kuna vitenzi vikuu, vitenzi visaidizi na vitenzi vishirikishi kama ilivyoainishwa na watalaamu mbalimbali katika isimu ya lugha kama vile Massamba na wenzake (ameshatajwa).
MAREJEO
Habwe, J, na Karanja (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.
Massamba, D.P.B na wenzake (2004), Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondari na Vyuo. TUKI: Dar es Salaam.
Mkude, D. J (1995) Uchunguzi wa Sentensiza Kiswahilikatika makala ya Lugha ya Kiswahili: Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili. TUKI: Dar es Salaam.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Matokeo kidato Cha pilibofya hapa
KUTAZAMA BOFYA HAPA <https://matokeo.necta.go.tz/ftna2020/ftna.htm>
-
Methali za kiswahili ---- Swahili proverbs 1. Adhabu ya kaburi aijua maiti, The touture of the grave is only known by the corpse 2. Akiba ha...
-
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM (DUCE) KITIVO CHA HUMANTIA NA SAYANSI YA JAMII IDARA YA LUGHA NA ISIMU JINA LA KOZI: ...
-
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHA DAR ES SALAAM (DUCE) KITIVO CHA HUMANITIA NA SAYANSI JAMII IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU KOZI: ...
Umejitahidi but unakopi kazi za semina hadi majina ya watu unaniangusha kaka
JibuFutapanga fresh bhana .unabananisha
JibuFuta