CHUO
KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHA DAR ES SALAAM (DUCE)
KITIVO CHA HUMANITIA NA SAYANSI JAMII
IDARA YA ISIMU NA LUGHA.
KOZI: FASIHI
ANDISHI YA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI: KF
202
KIONGOZI WA SEMINA: MADAM
GRACE
WASHIRIKI
|
NA
|
JINA KAMILI
|
NAMBA
|
PROGRAMU
|
SAHIHI
|
|
1
|
KIFYASI ONJENI WILLIUM
|
2014-04-05422
|
BAED
|
|
|
2
|
PASIANI EDINESTA INYASI
|
2014-04-05206
|
BAED
|
|
|
3
|
MLIMAKIFI HANZISTIN M
|
2014-04-05700
|
BAED
|
|
|
4
|
MWAZINI MIGISHA AUGUSTINO
|
2013-04-07105
|
BAED
|
|
|
5
|
KIDAVA SAYUNI NEHEMIA
|
2014-04-05428
|
BAED
|
|
|
6
|
SALIMU MONICA
|
2014-04-08120
|
BAED
|
|
|
7
|
YUNGE ISMAIL NKALI
|
2014-04-05722
|
BAED
|
|
|
8
|
SULLE VERONICA P
|
2014-04-05645
|
BAED
|
|
|
9
|
SERIKALI PILI
|
2014-04-07924
|
BAED
|
|
|
10
|
DAWSON EPIMARK
|
2014-04-07948
|
BAED
|
|
INSHA YA MUHULA.
“Suala la majaribio na mabadiliko katika
fasihi andishi ya Kiswahili halikwepeki”. Jadili kauli hii kwa kutumia kazi
mbalimbali za fasihi andishi ya Kiswahili
MPANGO KAZI
UTANGULIZI
Ø Maana ya fasihi andishi.
Ø Maana ya fasihi andishi ya Kiswahili.
KIINI
Ø Mabadiliko na majaribio katika
tamthiliya, Tiwaya, Hadithi fupi na Ushairi.
HITIMISHO
MAREJELEO
Maana ya fasihi
andishi imetolewa na wataalamu mbalimbali, kwa mujibu wa Wamitila (2003), ni
sanaa itumiayo maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa, pia
anasema fasihi andishi ina tanzu mbalimbali kama vile Riwaya, Tamthiliya na
Ushairi. Kwa mujibu wa www.shuledirect.co.tz/notes wanasema fasihi andishi ni tawi la fasihi
linalo tumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya
maandishi, zipo aina nyingi za fasihi andishi miongoni mwa hizo ni pamoja na
Ushairi, Riwaya, Hadithi fupi na Tamthiliya. Kwa ujumla tunasema fasihi andishi
ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno yaliyoandikwa ili kufikisha ujumbe kwa
hadhiira iliyokusudiwa. Fasihi andishi ya Kiswahili kwa mujibu wa Mulokozi
(1996) akiwanukuu Syambo na Mazrui (1992) fasihi andishi ya Kiswahili ni fasihi
iliyoandikwa kwa Kiswahili tu, iwapo inazungumzia utamaduni wa Kiswahili au
utamaduni mwingineo. Maadam fasihi hiyo imetumia lugha ya Kiswahili na imefuata
mbinu za ufasaha wa lugha hiyo basi kwa tafsiri yao ni fasihi ya Kiswahili. Kwa
ujumla fasihi andishi ya Kiswahili ni sanaa ya lugha iliyotungwa kwa lugha ya
Kiswahili na kuwasilishwa kwa hadhira (msomaji) kwa njia ya maandishi yenye
kuelezea utamaduni wa jadi ya Kiswahili. Hivyo basi zipo aina nne za fasihi
andishi ya Kiswahili kama vile Riwaya, Ushairi, Tamthiliya na Hadithi fupi.
Kwahiyo ni kweli suala la mabadiliko na majaribio katika fasihi andishi ya
Kiswahili halikwepeki kutokana na mabadiliko yanayotokea katika jamii ya
Kiswahili kama ifuatavyo;
Riwaya, Wamitila (2003) anasema kuwa
ni kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha, msuko
uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukua muda
mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalumu. Muhando na Balisidya
(1976) wanaeleza riwaya ni kazi ya kubuni, ni hadithi ambayo hutungwa kufuatana
na uwezo wa fanani kuibusha mambo kutokana na mazoea au mazingira yake. Hivyo
basi riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawanda mapana, lugha ya
kinathari, mchanganyiko wa visa na dhamira yenye kufungamana na wakati na
kushabihiana na maisha halisi na riwaya huwa na sifa kama vile masimulizi ya kubuni,
usimulizi wa kinathari, mpangilio wa msuko wa matukio, hufungamana na wakati,
urefu wakuanzia maneno 35000 na kuendelea na iwe na mawanda mapana.
Fasihi huithamini jamii kiitikadi,
kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii. Imekuwa ikibadilika badilika
kimtazamo fasihi nayo imekuwa ikibadilika kwasababu jamii nayo inabadilika.
Mabadiliko hayo katika riwaya (fasihi) kutokea kwasababu ya wasanii kutumia
vionjo vipya katika kuiumba kazi hiyo kama anavyosema Khamis (2007) mara moja tunaona neno kionjo linajisemelea
lenyewe kimya kimya juu ya mabadiliko ya utanzu wa fasihi. Mabadilko
yaliyotokea katika utanzu wa riwaya ni kama yafuatayo;
Kabla ya ukoloni, sehemu kubwa ya
riwaya ya Kiswahili ilikuwa ya kisimulizi (ngano, hekaya na tendi) baadhi ya
tendi hizo ni “Siri Asirari” (Binti
Temba 1863), “Kawaida ya Hamzia”
(1652) huu ulikuwa ni utenzi uliomsimfu mtume Muhhamed ulitungwa na Mwarabu
aitwaye Ali Hamzia. Katika kuandika riwaya za mwanzo waliweka misingi na
mitindo inayofuatwa na watunzi wa leo.
Wakati wa ukoloni, wakati wa utawala
wa Waingereza 1930 baada ya kuanzishwa shirika la uchapishaji la Afrika
Mashariki, East Africa Literature Bureau (EALB) shirika hili liliwahimiza
Waafrika kuandika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kuchapisha. Kipindi hiki kulikuwa
na mashindano ya uandishi wa riwaya za Kiswahili kutokana na mashindano hayo
waandishi wengi waliibuka na riwaya ya kwanza ya Kiswahili iliitwa “Uhuru wa Watumwa” iliandikwa na James
Mbotela 1885 na kilichapishwa 1934, “Mzimu
wa Kale” S. Abdallah 1960, “Simu ya Kifo” F. Katambula 1963. Riwaya zote hizo
zilichapishwa na shirika la uchapishaji la Afrika Mashariki (EALB) Riwaya za
wakati huo zilizungumzia kuhusu athari ya biashara ya utumwa na namna ya
kujikomboa na mfumo wa ukoloni na maadili mema.
Wakati wa uhuru (1961 hadi 1967),
Riwaya nyingi zilijadili juu ya ujenzi wa jamii mpya, madhara ya unyonyaji,
matabaka, athari za azimio la Arusha pamoja ba umuhimu wa elimu. Mfano wa
riwaya hizo ni kama vile “Dunia Uwanja wa
Fujo” ( E. Kezilahabi), “Njozi
Iliyopotea” Mung’ong’o miaka ya 1967-1980. Riwaya nyingi zilieleza
kuhusu umuhimu wa kuishi vijijini,
madhara ya vita, hali ngumu ya maisha, madhara ya ujamaa na unafiki wa viongozi
wetu mfano. “Miradi Bubu ya Wazalendo
(E. Ruhumbika), “Shida”, “Nyota ya Rehema”, “Kiu ya Haki”.
Kipindi cha 1980 hadi sasa, ni Riwaya
zinazojadili madhara ya rushwa, mapenzi, ndoa, matokeo ya ukoloni mamboleo
pamoja na mfumo wa kidemokrasia, mfano. “Mfadhili" (Hussein Tuwa), “Vuta N’kuvute” (Shaffi A. shaffi) na “Usiku Utakapokwisha” (Mbunda Msokile).
Utanzu mwingine ni Ushairi. Ushairi
umeelezwa na wataalamu mbalimbali wakitoa maana ya ushairi kama Amri (1954) ushairi au utenzi ni wimbo hivyo
anasema kama shairi haliimbiki halina maana. Shaaban Robert (1956) ushairi ni sanaa
ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tendi au tenzi. Kezilahabi
(1976) anasema kuwa ushairi ni tukio/ hali au wazo ambalo limeoneshwa kwetu
kutokana na upangaji mzuri wa maneno ya fasihi yenye mizani au uizani kwa ufupi
ili kuonesha ukweli Fulani wa maisha. Hivyobasi tunaweza kusema kuwa ushairi ni
sanaa ya lugha ya mkato inayosawili, kueleza au kuonesha jambo, kuonesha hisi,
au hali ya namna ya kuvutia katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa
uizani (mizani) wa sauti. Majaribio na mabadiliko katika ushairi wa Kiswahili
yanafafanuliwa na Wangai Mwai (2008:73) anasema fasihi hubadilika badilika
katika kumbo na maudhui kwahiyo ushairi wa Kiswahili sharti uruhusu mabadiliko
yanapotokea hivyo dunia inapobadilika na ushairi hauna budi kubadilika,
mabadiliko hayo yalitokea katika vipindi vifuatavyo kwa mujibu wa Kezilahabi
1983;
Muhula wa urasimu (0 hadi 1885) katika
muhula huu kanuni za utunzi wa ushairi ziliwekwa na zilitawaliwa na mitazamo ya
kidini na mamwinyi. Mfano kulikuwa na tendi nyingi zilizo ibuka huko Arabuni
wakati wa mtume Muhhamad mfano. “Shutaki
Anganwa”, “Nakaa”, “Masahibu” pia
kulikuwa na tungo za kitamaduni, mawaidha na tumbuizo mfano. “Utendi wa Mwanakupona” katika kipindi hiki pia kulikuwa na utawala wa
kiarabu, kilitawaliwa na fasihi ya kidini ambayo ilitafakari theolojia na
tafakari ya maisha.
Muhula wa utasa (1885 hadi 1945) katika muhula
huu ulikuwa wakati wamabaliko ya kiutawala, kielimu na kiuchumi. Hivyo mashairi
machache tu yalitungwa. Pia mabadiliko kutoka hati ya kiarabu kwenda ya kirumi.
Maandishi yaliyoandikwa yalikuwa ya Hemed Abdallah, Baadhi ya tenzi
zinazopatikana ni “Utenzi wa Vita vya
Majimaji” .Kanuni za uiandishi wa
mashairi zilianza kupotea.
Muhula wa urasimu mpya (1945 hadi
1965) hiki kilikuwa kipindi cha kufufua kanuni za utunzi. Shaban Robert, Amri
Abed, Khamis Aman na watalaamu wengine waliibua kanuni hizo za utunzi wa
ushairi. kipindi hiki ndipo kitabu cha kutunga mashairi kiliandikwa wakati
ambapo kilikuwa kinahitajika sana ilikuweka kiungo kizuri na wakati ulipo
(1954) mtindo uliotumika sana ni ule wa mizani 16, yaani nane kipande cha
kwanza na nane kipande cha pili ,
Muhula
wa sasa (1960 hadi sasa) Ni muhula wa kimutazamo mpya wa kimawazo na kisanaa.
Hivyo kuna mgogoro katika uwanja wa ushairi, Kati ya washairi wanaofuata uhuru
wa kisanaa. Hivyo mgogoro huu ulikuwa baina ya wanausasa na wanamapokeo ambapo
baadhi ya wanausasa ni kama Kezilahabi, M.M Mulokozi K.K Kahigi walianza
kuandika kazi za ushairi zisizo kuwa na urari wa vina na mizani. Wengi
walichukulia kushusha maendeleo ya ushairi lakini wanausasa waliona ni hatua ya
maendeleo. Hivyo mashairi yalitungwa kwa mfumo huo yaliapata majina kam vile
Makue, Mtiririko na Mapingiti.
Ibrahim Noor Shariff (1988:183) Amedai
kuwa mzozo uliibuka pale wanamabadiliko walipodai mambo matatu (3): Mbinu za
kutunga mashairi zilikuwa chache mno, sheria za kutunga mashairi ziliwanyima
uhuru watunzi kutunga na muundo wa tungo za kishairi ulikuwa wa Kiswahili hapo
zamani haukuwa na vina wa mizani. Hivyo sheria si za lazima. Kauli hizi za
wanamabadiliko zilipingwa sana na wanamapokeo ambao waliamini urari wa vina na
mizani ndiyo roho ya ushairi. Ruwaza ya
vina na mizani ndizo znafanya ushairi wa Kiswahili ujitambulishe. Njogu na Chimela
(1999:113) wanadai kwamba mgogoro huu ulikuwa kati ya vijana na wazee waliokuwa
wamekulia katika mazingira ya tungo za vina na mizani.
Tamthiliya (Wamitila 2002:7); Anasema
tamthiliya ni utungo unaoandikwa kwa mazungumzo, ambacho ni kipengele muhimu katika
tamthiliya. Mulokozi (1999) Anasema kuwa tamthiliya au drama ni fani ya fasihi
iliyokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili ya hadhira fulani. Ubora unaopatikana
katika maana hii ni kuwa imezingatia utendwaji jukwaa, hadhira, kusudio, na
fani iliyotendwa. Kwa ujumla, Tamthiliya ni utanzu wa fasihi unaotumia lugha ya
majibizano nyenye ubunifu wa hali ya juu ikiwa haina msisitizo wa uwasilishaji
wake jukwaani ili kufikisha lengo mahususi kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia
ya kuandikwa au isiyo ya kuandikwa. Sifa za tamthiliya ni kama vile dhana
inayotendwa, uwanja wa kutendea kazi, watendaji, hadhira, kusudio la kisanaa,
muktadha wa kisanaa na ubunifu. Mabadiliko yanayotokea kwenye utanzu wa
tamthiliya na kama ifuaytavyo;
Kabla ya ukoloni; tamthiliya ziliandikwa
ili ziigizwe jukwaani, hazikuwepo badala yake zilikuwepo ambazo hazikuandikwa
bali za kuigizwa kwenye shughuli mbalimbali kama vile jando na unyago, mazishi,
kwa mtemi, harusi na michezo ya watoto.
Sifa za tamthiliya hizo ni masimulizi (hadithi), wahusika, vitendo (utambaji),
daiolojia. Hata hivyo tamthiliya hizo hazikuwa na ki- Aristotle, wala hazikuwa
na matini zilizoandikwa, hivyo zilikuwa tamthiliya simulizi.
Kipindi cha ukoloni. Kipindi hiki
kilianza mwaka (1890 hadi 1960) hapa palikuwa na aina kuu mbili za tamthiliya
zisizo za kijadi. Tamthiliya za kizungu na vichekesho, mwishoni mwa kipindi
hiki palitokea aina nyingine ya tamthiliya ya kiswahili iliyoitwa tamthiliya ya
Kiswahili 1950. Aina hizi zimefafanuliwa kama ifuatavyo;
Tamthiliya za kizungu, Hizi
zilikusudiwa kuwaburudisha maofisa wa kizungu kama maseneta, kufundisha biblia
na kueneza imani ya kidini. Tamthiliya nyingi ziliandikwa kwa lugha ya
kiingereza na ziliigizwa shuleni, kiribu ya tamthiliya za kipindi hicho
zilikuwa za kibwenyenye (maisha ya starehe) tamthiliya chache sana ziliandikwa
kwa Kiswahili mfano , ‘Tabibu Asiyependa
Utabibu’ kimeandikwa na A. Marrison.
Vikundi vingi vilianzishwa kwa ajili ya kuigiza tamthiliya ya kizungu mfano Dar es Salaam players (little theatre) 1947
na Arusha little theatre Musuka 1953.
Vichekesho;
Ni aina ya tamthiliya geuzwa yaani
hutungwa papo kwa papo bila kuandikwa.
Tamthiliya hizi zilianza miaka ya 1920 kwa lengo la kuburudisha wenyeji.
Tamthiliya nyingi zilikuwa na vituko vya kuchekesha na zilijenga kuigiza kuhusu
ushamba, ujinga na kutokuwa msitaarabu.
Tamthiliya hizi zilimuonesha mhusika
anaetoka shamba na kwenda kuzurula mjini kutafuta kazi. Ziliendelea mpaka baada
ya uhuru ila hivi sasa maudhui yake yamebadilika.
Tamthiliya
andishi ya Kiswahili; hizi ziliandikwa kabla ya kuigizwa jukwaani na zilianza
kutokea miaka ya (1950). Mfano Imekwisha
ya C.Frank,(1951), Tamthiliya
nyingi za kidini zilindikwa mashuleni na kanisani tu lakini hazikuchapishwa
vitabuni. Mfano Karibu Mgeni ya Graham Hyslop (1957). Pia mwaka
huo aliandaka kitabu cha Afadhari Mchawi,
Nakupenda
Lakini…. ya Henry Kuria (1954), Nimelogwa
nisiwe na Mpenzi ya Gerishon Ngugi (1961). kwa ujumla hadi tunapata uhuru
tamthiliya zilikuwa zimeandikwa na Wakenya.
Kipindi
cha uhuru hadi sasa; Tamthiliya ya kizungu iliendelea kuigizwa mashuleni na
katika kumbi maalumu za maonyesho (Little theatres)baadhi ya tamthiliya maarufu
zilitafsiriwa na kuigizwa ni za Julius Kaizali (Shakespear),Mabepari wa Venis ya JK. Nyerere(1969),Mfalume Edipode , Mchuuzi muungwana, Pia
tamthiliya za Kiafrika zilizo tafsiriwa na kama Mtawa mweusi(The black
Hermit)ya Ngugi wa Thiongo ,Nitaolewa Nikipenda (I will Merry when I want) ya
Ngugi wa Thiongo na Ngugi wa Mini (1982). Kipindi hiki kimegawanyika katika vipengele viwili ambavyo
vimefafanuliwa kama ifuatavyo;
Vichekesho; vichekesho viliwasuta wazungu weusi wanaoishi
maisha ya kizungu, waliolingia elimu na vyeo vyao na kudharau
wengine,Vilevile vilijadili matatizo ya
kijamii, ukosefu wa kazi, Ukimwi, Uhalifu, udanganyifu wa waganga wa kienyeji.
Pia kulikuwa na vichekesho vya kisiasa ,ujamaa na ubinafsi wa viongozi ambao
ambao sasa umetawala na Mtatizo ya kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa. Mfano
kipindi cha Mahoka kilianzishwa mwaka (1974) Pwagu na Pwaguzi. Walikuwa
wanachekesha Redio Tanzania vilikejeli baadhi ya tabia za viongozi na sera za
Azimio la Arusha
Tamthiliya
andishi ya Kiswahili; utanzu huu ulichochewa zaidi na mashindano yailiyoongozwa
na chama cha waigizaji wa vijana Tanzania. Watanzania wengi walianza
kuandika tamthiliya za Kiswahili. Mfano
“Wakati Ukuta”ya Ibrahim
Hussein(1969). Tamthiliya hii ilishinda mashindano na kupewa tuzo, Kinjekitile ya Ibrahim Hussein (1969),
pia Kaptula la Marx ya E.Kezilahabi.
Tamthiliya andishi ya Kiswahili ilikuwa na maudhui ambayo twaweza kugawa
tamthiliya ya Kiswahili kutoka mwaka 1960 hadi sasa kama vile;
Tamthiliya
zinazoelezea migogoro ya utamaduni kati ya ukale na usasa, Mfano Nimelogwa nisiwe na Mpenzi ya Ngugi
Gerishoni. Pia matatizo ya kijamii kama mapenzi, ndoa, ufukara na Urithi. Mfano
Mke Mwenza, Nakupenda Lakini…, pia
kuna tamthiliya za kidini zinazoelezea matatizo ya kidini zilizo ingia moja kwa
moja toka ulaya. Mfano Aliyeonja Pepo
ya F.Topari, ukombozi wa kitaifa hizi ni tamthiliya zinazoonesha harakati za
ukombozi wa ukoloni pamoja na ukombozi wa Nyanja zote za maisha. Mfano Tone la Mwisho ya Emmanel Mbogo. Na
mwisho walilenga ujenzi wa jamii mpya, Mfano
Giza limeingia ya Emmanuel Mbogo na Kijiji chetu ya Ngaliyoma.
Hadithi
fupi; Kwa mujibu wa Wamitila (2002:68) Hadithi fupi ni utungo mfupi wakinathari
unaojishughilisha na suala fulani kuu, wenye wahusika ambao hawakuzwi, Na
unaoutumia mbinu za kimaelezo za
kibunifu, zenye uelekezi wa kiwango cha juu. Kwa mujibu wa Msukile(1992), Ni
aina ya kazi ya sanaa ya utanzu wa hadithi inayotumia lugha iliyoandikwa kinathari au iliyo katika
masimulizi kama haijaandikwa. Kwa ujumla hadithi fupi andishi ya Kiswahili; Ni
aina ya kazi andishi ambayo huwa fupi na huangazia wazo moja na kurejea kisa kimoja, Pia huwa na wahusika
wachache na huchukua muda mfupi, hadithi fupi huwa na sifa kama vile kuwa
na athari za aina moja, urefu wa kusomeka kwa mkao mmoja na itumie lugha
iliiweze kuleta mguso wa kihisia na si kiakili.
Hadithi
fupi andishi ya Kiswahili inabainishwa na Brander Methew anaye aminika kutumika
neno la kiingereza Short story na
kuonesha yeye nimiongoni mwawaasisi wa utanzu wa utanzu huu wa fasihi. Chimbuko
la hadithi fupi ni masimulizi ya kijadi ambayo yanahusisha ngano, hekaya tendi
na rara. Pia hadithi fupi andishi ya Kiswahili imetokana na hadithi fupi za
kigeni. Mabadiliko na majaribio hayo yamejitokeza katika vipindi vifuatavyo:
Miaka
ya (1960) hadi (1970); kipindi hiki hadithi fupi ziliandikwa magazetini, Mfano
gazeti la Mzalendo, Kiongozi, Mamboleo, Nchi nyetu na gazeti la Afrika
Mashariki. Pia kipindi hiki mashindoni ya kuandika hadithi fupi andishi yaliandaliwa. Miongoni
mwake ni Chamnyonge utakipata Hadharani,
Mayai Waziri wa Maradhi. Hatimaye zikaanza kusemwa redioni, mfano shirika
la utangazaji la Britsh Broadcasting Cooperation (BBC). Baadaye zikaandikwa
vitabuni ikiwa nimfululizo wa vitabu mbalimbali, mfano Pavumapo palilie na Kimya
jumba la Maneno.
Miaka
ya (1970) hadi (1980); katika kipindi hiki waandishi wengi walijitokeza kuandika hadithi fupi mbalimbali, mfano Nitakuja kwa Siri na Kimya jumba la Maneno .
Miaka
ya (1990), kipindi hiki hadithi fupi za Kiswahili zilidumaa kwa sababu
waandishi wengi waliandika hadithi zenye dhamira za kufanana na wasomaji wengi
walipuuza kwasababu hadithi nyingi ziliingiliana.
Miaka ya ( 2000) hadi sasa; Jitihada za uaindishi wa hadithi fupi
zilianza tena na vitabu vingi viliandikwa na kukusanywa, hii ilitokana na
mabadiliko ya utandawazi waandishi wengi walianza kuandika athari za utandawazi,
mfano kitabu cha Mwendawazimu cha
Mbatia, Mayai Waziri wa Maradhi na
hadithi nyingine katika kitabu cha Wamitila.
Hivyo basi fasihia andishi ya
Kiswahili hubadilika kutokana na mabadiliko katka jamii. Hivyo kuna sababu
ambazo hupelekea mabadiliko haya kama vile ugunduzi wa teknolojia ya upigaji
chapa wa vitabu, ukuaji wa shughuli za kiuchumi, mageuzi ya kijamii na kisiasa
yaliyofungamana na mabadiliko ya kiuchumi na sababu nyinginezo ndizo
zilizosaidia kuleta mageuzi makubwa katika kazi ya Fasihi andishi ya Kiswahili.
MAREJELEO
Abedi,
A. (1954) Sheria za Kutunga Mashairi na
Diwani ya Amri. Nairobi: EALB
Chawakamamnma. Blogspot.com
Msokile,
M. (1992). Misingi ya Hadithi Fupi,
Dar es salaam: Dar es salaam University
Press.
Muhando, P na Balisidya, M. (1976) Fasihi na Sanaa za Maonesho. Dar es salaam:
TPH
Mulokozi, M,M. (1996), Utangulizi
wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es salaam: Chuo Kikuu Huria, (ukur 1-93, 229-230).
Samwel,
M & Akech, J (2013) Diwani ya MEA. Moveli
publishers: Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni