Jumanne, 4 Oktoba 2016
tafsiri na ukalimani
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM
(DUCE)
KITIVO CHA HUMANTIA NA SAYANSI YA JAMII
IDARA YA LUGHA NA ISIMU
JINA LA KOZI: TAFSIRI NA UKALIMANI
MSIMBO WA KOZI: KI311
MKUFUNZI WA KOZI: CHIPALO AMANI
AINA YA KAZI: SEMINA
SIKU YA SEMINA: JUMATATU, SAA: 4:00 ASUBUHI
WAHUSIKA
NA JINA NAMBA ZA USAJILI PROGRAMU SAINI
1 KOMBA FREDRICK 2014-04-05576 BAED
2 MLIMAKIFI HANZISTIN2014-04-05700BAED
3 NDUNGURU STELA 2014-04-05648 BAED
4 NYIWALA JANE 2014-04-07968 BAED
5 KASSANGA PUDENSIANA2014-04-05404BAED
6 KIDAVA SAYUNI 2014-04-05428 BAED
7 PASIANI EDINESTA 2014-04-05206 BAED
8
MPANGO KAZI
UTANGULIZI
Maana ya Semantiki kwa mujibu wa walaalamu.
Maana ya Fahiwa, Utajo na Urejeleo.
KIINI
Kufanana na kutofautiana kwa “utajo”, “Urejeleo” na “Fahiwa”.
Jinsi dhana hizi zinavyofanikisha au kukwamisha kupata maana katika lugha
HITIMISHO
MAREJELEO
Baadhi ya wataalamu wamejaribu kutoa fasili ya Semantiki kwa kuzingatia vipengele mbalimbali kama ifuatavyo;
Lyons (1968) anasema “Semantiki ni taaluma ya maana”.
Udhaifu wa fasili hii ni kwamba mtaalamu huyu hajaelezakuwa maana hiyo imejikita katika kipengele gani, je kipengele cha maneno au sentensi.
Masamba (2004:75) anasema “Semantiki ni taaluma ya isimu inayojishughulisha
na uchambuzi na uchunguzi wa maana ya maneno na tungo katika lugha”
Kwa ujmula, Semantiki ni taaluma inayojushughulisha na uchambuzi na uchunguzi wa maneno au viambajengo vya maneno au leksimu katika lugha. Taaluma hii inadhana za msingi zinazotumika kurejelea maana katika lugha. Zifuatazo ni dhana hizo ambazo ni “Utajo”, “Urejeleo” na “Fahiwa’;
Utajo, Lyons (1977)anasema “Ni uhusiano kati ya leksimu na seti ya vitu
ambavyo vinarejelewa na leksimu hiyo”.
Dhana hii inatokana na neno taja au kutaja. Uhusiano huo hurejelea vitu kwa majumui. Mfano kiyambo pombe hurejelea pombe za aina zote duniani, mfano watu wakiwa baa mmoja akitaja pombe ataulizwa pombe gani kwani neno hilo linataja aina zote za pombe ulimwaenguni. Pia neno chakula hurejelea hurejelea vakula vyote kama ugali, wali, pilau na viazi.
Urejeleo,Yule (1996:17) “Ni kitendo cha mzungumzaji au mwandishi kutumia
alama za kileksimu kumuwezesha msomaji au msikilizaji kutambua kitu kinachosemwa”.
Kwa ujumla, urejeleo ni uhusiano baina viambo vya lugha na na viwakilishi vyake duniani, wakati maalumu wa semo na mkutadha, urejeleo huweza kutaja kitu mahususi, Mfano kama hapa chini;
Chakula ugali, wali, pilau na viazi
Pombe bia, mbege, chibuku na ulanzi
Nyama ya kuku, ya mbuzi ya bata na nyama ng’ombe
Katika mifano hii tunaona kuwa maneno yaliyokiolezewa wino ni maneno mahususi yanayorejelewa na leksimu kuu. Mfano mzungumzaji akitaka kutaja kitu lazima ataje kitu mahususi.
Fahiwa, Matinde (2012:261) anasema “Ni dhana ya leksimu inayowakilishwa
na neno tofauti na kirejelewa chenyewe”.
Hivyo tunaweza kusema fahiwa ni mahusiano yaliyopo baina ya kiyambo kimoja na viambo vingine katika lugha, mahusiano hayo huitwa mahusiano ya kifahiwa. Ifuatayo ni mifano ya mahusiano ya kifahiwa;
Usinonimia, ni hali inayojitokeza au iliypo pale ambapo maneno mawili au zaidi yenye maumbo tofauti na maana moja au inayokaribiana. Maneno hayo huitwa sinonimia au viswe. Mfano: fedha, hela na pesa.
Mjinga, bwege na mpumbavu
Jembe, mchizi, mshikaji na msela.
Mifano hii inaonesha maumbo tofauti yenye maana zinazo karibiana.
Uantonimia au unyume, ni uhusiano wa kimaana baina ya maneno mawili ambapo maana ya neno moja ni kinyume cha nenolingine, uhusiano wa maneno hayo huitwa antonimia. Mfano nyuma inakuwa mbele, mwanamke inakuwa mwanaume, kubwa inakuwa ndogo.
Umeronimia, ni uhusiaono ulipo baina ya leksimu inayotaja sehemu ya kitu na leksimu inayotaja kitu kizima, mfano mwili sehemu zake ni kichwa, mihuu, mikono, mabega na tumbo pia ukitaja kichwa kuna macho. Masikio, mdomo na nywele.Hiyo ni mifano kadhaa inayoonesha mahusiano ya kifahiwa katika luhga. Ufuatao ni ufanano uliopo baina ya “Utajo”, “Urejeleo” na “Fahiwa”;
Zote ni dhana za muhimu zinazodokeza maana kwa undani zaidi. Mfano ukitaja rangi na baadae ukataja aina mahususi kama njano, bluu na nyekundu basi inamsaidia mtu kupata maana mahususi, pia fahiwa husaidia kupata maana kwa kutumia neno kulingana na mahitaji yake, mfano katika unyume.
Pia zote husaidia katika ujifunzaji wa lugha, mfano wakati wa kumfundisha mtoto mdogo tunataja neno pamoja na kirejeleo chake kama ukisema kiti basi unamuonesha kiti hicho, pia katika maneno kama kisu, jembe na embe ukimtajia basi unamuonesha virejelewa vyake. Zifuatazo ni tofauti zilizopo katika dhana hizo;
Utajo hurejelea vitu kwa ujumla au majumuhi, mfano nyumba au chakula bila kutaja aina zake lakini urejeleo hutaja vitu mahususi, mfano katika chakula urejeleo hutaja aina mahususi ya chakula lama vile ugali, wali na viazi, pia katika pombe basi hutaja aina mahususi ya pombe.
Fahiwa huweza kuibua utata katika maneno lakini urejeleo hauibui utata katika maneno, katika fahiwa uhomonimia huweza kuibua utata kama msemaji au mwandishi hatazingatia mkutadha,mfano katika maneno haya;
Kaa –mdudu
Kuketi
Moto
Ganda la kibiriti
Panda – weka mbegu aridhini
kwea
Mgawnyo wa njia mbili
Zifuatazo ni namna dhana hizi zinavyoweza kufanikisha maana katika lugha;
Dhana ya utajo hufanikisha maana katika lugha kwa kutaja vitu au maneno kimajumui, kupitia dhana hii humsaidia mtumiaji wa lugha kupata maana kwa ujumla. Mfano kujua matunda kama neno majumuhi baadae atajua aina zake.
Urejeleo humsaidia mtumiaji wa lugha kupata maana mahususi kwani hutaja neno na kurejelea kitu mahususi katka mkutadha huo. Mfano ukitaja meza lazima utataja aina mahususi kama meza ya chuma, meza ya mviringo, meza ya mbao.
Fahiwa inafanikisha kupata maana za maneno yenye maumbo tofauti tofauti yenye uhusiano kimatumizi lakini katka mkutadha fulani au maalumu na pia maana ya neno katka seti kuu. Mfano; pesa, hela na fedha.
Tundu, shimo na tobo.
Fahiwa humsaidsia mtumiaji wa lugha kupanua maana au kukuza lugha, kwa kupitia uantonimia, mtu apatao dhana au maana ya neno panga ni rahisi kwake kujua maana ya neno pangua kwa kuwa maneno haya yana maana kinzani. Zifuatazo ni namna dhana hizi zinavyoweza kukwamisha maana katika lugha;
Katika urejeleo kuna maneno mengine hayana virejeleo maalumu mfano maneno kama viunganishi, vivumishi nivigumu kupata vireleleo nyake hivyo basi yakisimama peke ni vigumu kupata maana. Pia kuna dhana kama Mungu, malaika na shetani ni vigumu kupata virejeleo vyake.
Baadhi ya dhana huweza kusababisha utata katika lugha, mfano utajo huweza kuleta utata kwa sababu kitajwa chake si mahususi. Kama mtu akitaja meza bila kutaja aina muahususi ya meza hiyo itamuwia vigumu msikilizaji au msomaji kupata maana kamili. Hata fahiwa husababisha utata hasa pale mtu anapotumia neno lenye maana zaidi ya moja kama vile shuka, lia na panda, maneno haya huleta utata katika kupata maana.
Kwa ujumla, kiatika Semantiki dhana hizi hutumika katika lugha ili kupata maana, pia dhana hizi hutegemeana kulingana na matumizi yake katika lugha, kwa kutumia nadharia mbalimbali za maana na aina za maana hujumuisha katika upatikanaji wa maana katika lugha.
MAREJELEO
Lyons, J (1968). Introduction to Theoretical Linguistic. New York: Cambridge University Press.
Liyons, J (1977). Semantics. Great Brutain: Cambridge UNiveristy Press
Masamba, P. B. D (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI
Yule, G (1996). Pragmatics. New York: Oxford University Press.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Matokeo kidato Cha pilibofya hapa
KUTAZAMA BOFYA HAPA <https://matokeo.necta.go.tz/ftna2020/ftna.htm>
-
Methali za kiswahili ---- Swahili proverbs 1. Adhabu ya kaburi aijua maiti, The touture of the grave is only known by the corpse 2. Akiba ha...
-
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHA DAR ES SALAAM (DUCE) KITIVO CHA HUMANITIA NA SAYANSI JAMII IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU KOZI: ...
-
DAR ES SALAAM UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION (DUCE) WAKOLONI WALILETA ELIMU AU MASOMO? Hoja yangu ya wiki iliyopita ni kwamba...
Angalau mngesema neno jema
JibuFuta