CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU CHA DAR ES SALAAM (DUCE)
KITIVO CHA HUMANITIA NA SAYANSI JAMII
IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU
KOZI: FONOLOJIA YA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI: KI 208
KIONGOZI WA SEMINA: MICHAEL A MASHAURI
CHUMBA CHA SEMINA: LR/A
SIKU YA SEMINA: JUMATANO
MUDA WA SEMINA: SAA 5:00 -5:55 ASUBUHI
WASHIRIKI
NA
JINA KAMILI
NAMBA
PROGRAMU
SAHIHI
1
2014-04-0
BAED
2
2014-04-
BAED
3
MLIMAKIFI HANZISTIN M
2014-04-05700
BAED
4
MAGUKU DENES MAGOMBA
2014-04-05195
BAED
5
KIDAVA SAYUNI N
2014-04-05428
BAED
SWALI LA 2:
Fafanua fonolojia ya lugha ya Kiswahili.
MPANGO KAZI
UTANGULIZI
Maana ya fonolojia
Maana ya fonimu
KIINI
Vipengele mbalimbali vya fonolojia
HITIMISHO
MAREJELEO
Kwa mujibu wa TUKI (1990) Anasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushugulikia uchambuzi wa sauti zinazotumika katika mfumo fulani. Mgullu (1999) Akimnukuu Hartman 1972 anasema kwamba fonolojia ni mtalaa wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani na uamilifu wao ndani wa mfumo lugha inayohusika. Massamba na wenzake (2004) Wanasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaljishughulisha na uchambuzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za binadamu. Kinachosemwa hapa ni kwamba fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahsusi. Hivyo kipashio cha kifonolojia ni fonimu. Fonimu kwa mujibu wa Daniel Jones (1967) Wanasema kuwa ni kipashio kidogo zaidi cha mfumo wa sauti ambacho hutumika kubainisha maana za maneno mawili ya lugha moja. Massamba (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi kuweza kukitofautisha na a vipande vingine vya aina yake. Massamba na wenzake (2004) Wanasema fonimu ni kitamkwa kilichobainifu katika lugha fulani maalumu. Hivyo tunaweza kusema kuwa fonimu kipashio kidogo ch kifonolojia kinachoweza kuweza kubadili maana ya neno katika lugha fulani (mahususi).
Mfano pata bata
Kura kula
Oa ua
Hivyo basi fonolojia inajihusisha na vipengele vikuu viwili ambavyo ni vipande sauti na vipengele arudhi. Vipande sauti ni kipengele ambacho kinashughulikia uchunguzi wa vipande vyenyewe, wanaisimu katika aina hii hubainisha vipande sauti bainifu katika lugha kama vile alofoni na fonimu pia kueleza fonimu hizo jinsi zinavyoweza kuathiriana katika maneno mbalimbali. Vipande sauti hivyo ni irabu na konsonanti. Irabu kwa mujibu wa Massamba na Wenzake (2004) anasema irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi na kuwepo kizuizi chochote katika mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywa na chemba ya pua. Hii ina maana kuwa irabu zote ni ghuna. Hivyo lugha ya Kiswahili inazo jumla ya irabu tano (5) ambazo ni i,e,a,o na u. na vipo vigezo vikuu viatu vinavyo tuongoza kubaini/ kuainisha irabu kama vile mahali pa kutamkia, mwinuko wa ulimi, na hali ya midomo.
Mahali pa kutamkia. Irabu huweza kutamkwa katika sehemu tatu za ulimi. Sehemu
MBELE KATI NYUMA
/i/ /u/
/ԑ/ /ᴐ/
/a/
Mwinuko wa ulimi. Katika sifa hii kinachoangliwa ni jinsi ulimi unavyoinuka yaani kama irabu ya chini irabu inapotamkwa ulimi upo chini. Irabu ya kati ulimi unakuwa kati na irabu a juu ulimi unakuwa juu.
/i/ /u/ JUU
/ԑ/ /ᴐ/ KATI
/a/ CHINI
Hali ya midomo. Hapa sifa hii inaangaliwa kama midomo imeunda umbo la mviringo au haijaunda yaani ipo mtandazo. Hivyo tuna sifa viringe na si viringe. Tafiti zinaonesha kuwa irabu za mbele hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa, lakini irabu za nyuma hutamkwa midomo ikiwa mviringo.
irabu
Sifa kutokana na hali ya midomo
i, ԑ
Irabu si viringe
ᴐ,u
Irabu viringo
Konsonanti kwa mujibu wa Massamba na wenzake(2004) wanasema ni sauti ambazo katika utamkaji wake mkondo hewa huzuiwa kutoka mapafuni kupitia katika chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Uzuiwaji wa mkondo hewa unaweza kuwa wa kubana au kuachiwa taratibu kama kutamka sauti /ch/. Wikipedia.org/wiki/Matumizi ya lugha. Anasema kuwa konsonanti zinapotamkwa hewa huzuiliwa na ala za matamshi. Kuna vigezo vikuu viwili vinavyotumika kuainisha konsonanti za lugha ya Kiswahili ambazo ni
Mahali pa kutamkia, hapa kinachoangaliwa ni konsonantiimetamkwa wapi kama ni konsonanti ya meno, ufizi, midomo. Konsonanti za midomo ni [m], [p],[b]. konsonanti za midomo meno kam vile [f] na [v]. konsonanti za meno hizi hutamkwa kwa kutumia meno ya juu na ncha ya ulimi sauti kama [θ] na [ð], konsonanti za ufizi, hizi hutamkwa kwa kutumia ufizi mfano wake ni sauti kama vile [n], [t], [d], [s]. konsonanti za kaakaa gumu, hizi ni konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake hutegemea sehemu ya juu ya chemba ya kinywa kama vile [ʧ] na [j], konsonanti za kaakaa laini, hutamkwa katika sehemu inayoanza na mara baada ya kaakaa gumu [k], [g], [ŋ]. Konsonanti za glota, hizi ni aina ya konsonanti ambazo hutamkiwa katika koromeo mfano [h]
Hali ya mkondo hewa, kinachoangaliwa hapa ni namna ya utamkaji yaani hli ya mkondo hewa kuzuiwa moja kwa moja na kuachiwa ghafla, kuzuiwa kidogo na kuachiwa ghafla, hewa hewa kutoka kwa kukwama kwama, aina hizo ni pamoja na: vipasuo hizi ni aina ya konsonanti ambazo wakati wa utamkajihewa kutoka mapafuni hubanwa na kuachiwa ghafla. Kama vile [b], [k], [g]. vipasuo kwamizi, hewa huzuiwa na kuachiwa polepole na kupita kwa kukwama kwama kama vile [ʧ], [j], vikwamizi hizi ni konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake hewa huzuiwa na kuachiwa kupita katika nafasi ndogo ya ala za sauti zilizo karibiana na hivyo hewa kupita kwa kukwaruza mfano [θ], [f], [v] na [z]
Hali ya nyuzi sauti, kinachoangaliwa hapa ni kama nyuzi sauti zinatikiswa na hivyo kurindima na kutoa mghuno au hazirindimi na hivyo hazitoi mghuno. Ghuna nyuzi sauti hurindima na kutoa mghuno mfano [b], [g], [n], [ŋ]. Konsonanti si ghuna ni zile ambazo nyuzi sauti hazirindimi kama vile [f], [θ] [h], [s].
Sifa bainifu za fonimu, hizi ni kama zifuatazo;
Usilabi, sifa hii huainisha fonimu yenye sifa ya kuwa na usilabi na ambaz hazina sifa hiyo ya lugha yakiswahili sanifu. Irabu zote pamoja na nazali katika mazingira maalum huwa na sifa a usilabi na zilizobaki yaani konsonanti zote na nazali huwa hazina usilabi [+sil].
Mfano mtoto $m $to $to $
Sifa ya mghuno yaani mtetemo wa nyuzi sauti. Sifa hii huainisha fonimu za Kiswahili zile zenye mghuno na zisizo na mghuno. Irabu zote ni ghuna, nazali na viyeyusho.
Mfano [a], [i], [m], [y]
Sifa ya mwachano taratibu taratibu [±tar] sifa hii ni sauti inayotolewa wakati hewa ikiachiwa taratibu.
Mfano ch [ʧ]
Unazali, nazali zote zina sifa ya unazali [+naz] vitamkwa vinavyobaki havina sifa hiyo.
Mfano: [m], [n], [ŋ].
Ukontinuanti, [±kont] sifa hutumika kubainisha sauti ambazo zimetamkwa wakati mkondo hewa ukiwa wazi bila kuzuiliwa mahali popote.
Mfano: irabu zote na nazali.
Umadende, [±mad] sifa hii hutumkika kwa ala sogezi kugonga gonga kwa haraka kwenye ufizi.
Mfano: [r] rudi
Sifa za mahali pa matamshi
Uanteria. Sifa hii inahusu vitamkwa kuanzia kwenye ufizi kwenda mbele yaani ufizi [d], meno [f], midomo [b] na [m].
Umeno, sifa hii inahusu vitamkwa ambavyo hutamkwa wakati ulimi ukiwa katikati ya meno.
Mfano: [ð], [Ɵ]
Dhambi, Thamani,
Kanuni za michakato ya kifonolojia.
Uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho (w) na (y) irabu yeyote ya juu ( iwe /i/ na /u/) ikifuatana na irabu isiyo fanana nayo katika neno irabu hiyo hubadilika na kuwa kiyeyusho.
Mfano: umbo la ndani umbo la nje
/mu+isho/ [mwi:sho]
/Mu+anzo/ [mwa:nzo]
/mu+embe/ [mwe:mbe]
Hapa tunaona wazi kwambi katika lugha ya Kiswahili, irabu ya juu nyuma /u/ hubadilika na kuwa kiyeyusho/w/ kutokana na kufuatiwa na irabu ambayo haifanani nayo mchakato huu unaweza kuoneshwa na sheria/ kanuni ifuatayo.
/u/ [w] I ≠ u
Pia katika kuunda kwa kiyeyusho /j/ mfano ni kama ifuatavyo,
Umbo la ndani umbo la nje
/Mi+ezi/ /mje:zi/
/vi+ungu/ vju:ungu/
Katika mifano hii huona wazi kwamba irabu ya juu mbele imebadilika na kuwa kiyeyusho /j/ kutokana na kufuatiwa na irabu ambayohaifanani nayo mchakato huu unaweza kuoneshwa na
/i/ [j]/ I ≠ i
Ukakaishaji, kwa mujibu wa Massamba (ametajwa) anasema ukakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu ni sifa zisizo za kaakaa gumuzinapobadilika na kuwa za kaakaa gumu. Lugha ya Kiswahili ina fonimu mbili za kaakaa gumu ambazo ni /j/ na /ʧ/ maelezo hayo yanaweza kuthibitishwa na mifano kutoka katika lugha ya Kiswahili.
Umbo la ndani umbo la nje
/ki+ angu/ [cha:ngu]
/ki+ombo/ [cho:mbo]
Mchakato huu unaweza kuoneshwa kanuni ya kifonolojia ifuatayo.
/k/ [ʧ]/ i + I ≠ /i/
Hata hivyo kanuni inaweza vigairi kama inavyothibitika katika miufano ifuatayo.
Umbo la ndani umbo la nje
/ki+ oo/ [choo]
/ki+ atu/ [chatu]
Udondoshaji wa irabu, ni mchakato wa kifonolojia ambapo irabu inadondoshwa wakati ambapo jambo moja mojawapo kati yafuatayo yanapotokea. Wakati ambapo irabu inafuatiwa na konsonanti ya kweli na wakati ambapo irabu zinafuatana
Mfano: Umbo la ndani umbo la nje
/mu+zigo/ [mzigo]
/mu+ dogo/ [mdogo]
Katika data hii tunaona kwamba irabu /u/ inadondoshwa inapofatiwa na konsonanti ya kweli. Mchakato huu unaweza kubainishwa na kanuni ifuatayo.
U [Ɵ]/ /m/ K (halisi)
Pia irabu inaweza kudondoshwa ikifuatana na irabu nyingine kama inavyoo nekana katika mifano ifuatavyo;
Umbo la ndani umbo la nje
/wa+limu/ [walimu]
/Wa+angu/ [wangu]
Mchakato huu unaweza kuwakilishwa kwa kanuni ifuatayo
/a/ [Ɵ] ⁺ [a]
Yaani irabu /a/ inadondoshwa katika mazingira ambapo inafuatiwa na irabu inayofanana katika mpaka wa mofimu
Usimilisho pamwe wa nazali; katika mkururo huu wa nazali na konsonati, nazali huathiriwa na konsonati inayofuata. Usimilisho huu hutegemea mahali ambapo konsonati hiyo hutamkiwa. Hapa nazali hupewa umbo jumuishi /N/.
Mfano ; Umbo la ndani umbo la nje
/n+buzi/ [mbuzi]
Hivyo mchakato huu unaweza oneshwa kwa kutumia kanuni hii ifuatayo
/N/ [m]/ /b/
Fonimu jumuishi (N) inajitokeza kama [m] katika mzingira ya kufuatiwa na [b]
Kuimarika kwa fonimu;pale ambapo fonimu hafifu hubadilika nakuwa na kuywa yenye nguvu ,kuimarika kwa fonimu ni kule kuongezeka kwa nguvu za misuli na msukumo wa mkondo hewa wakati wa utamkaji fonimu husika
Mfano Umbo la ndani umbo la nje
/n/+refu/ [ ndefu]
/n+limi/ [ndimi]
Kwa kutumia mifano hiyo tunaona wazi /r/na /l/ zinabadilika na nakuwa /d/ pale zinapotanguliwa na nazali ya ufizi /n/ ,mchakato huwa kama ifuatavyo ;
r
l [d] N
Kudhohofika kwa fonimu; hapa fonimu iliyokuwa ikitamkwa kwa nguvu hutumia sauti nguvu kidogo,
Mfano; Umbo la ndani umbo la nje
/mpendi/ [mpenzi]
/ Mpiki/ [mpishi]
Hapa tunaona wazi kuwa /d/ hubadilika na kuwa [z] na /k / kuwa/ /pale zikifuatiwa na irabu i yaunominishaji mchakato huo ni huu ;
d z I ya unominishaji.
k
Pia folojia hushughulikia vipengele arudhi katika lugha vipengele arudhi ni vipengele vya fonolojia vinavyoshughulikia sifa zaidi ya vipande sauti. Vipengele arudhi ni kama vile
mkazo, ni utamkaji wa nguvu zaidi katika sehemu ya neon au fungu la maneno, utamkaji huu hufanywa katika silabi na hutokea katika silabi ya pili kutoka mwisho katika lugha ya Kiswahili.
Mfano: mwali’mu
Hayu’po
Mzu’ri
Kiimbo, kwa mujibu wa Massamba na wenzake (2004) ni kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti. Katika lugha ya Kiswahili, kiimbo hutusaidia kuelewa au kubaini lengo la msemaji kama vile;
kutoa maelezo (-) mfano. Atafika leo mchana
kuuliza swali (/) mfano. Kwanini?
kutoa amri (/) mfano. Ondokeni hapa.
Lafudhi, ni sifa yakimasikizi ya matamshi ya mtu binafsi ambayo humpa msemaji utambulisho fulaniwa kijamii au wa kieneo. Katika lugha ya Kiswahili, lafudhi hutufanya tuweze kutofautisha kati ya watu wa pwani na bara. Hii inatokana na athari ya lugha za mwanzo yaani lugha mama, watu wa bara Kiswahili ni lugha yao ya pili wakatti watu wa pwani ni lugha yao ya kwanza.
Kiswahili sanifu. Kiswahili cha kusini
Mtoto anaumwa. Ntoto anaumwa.
Toni, Mgullu (1999) Anasema toni ni kiwango cha kidatu pamoja na mabadiliko yake ambayo hutokea wakati mtu anpotamka silabi au maneno. Katika lugha zenye toni mabadiliko yake hubadili maana za maneno. Ila katika lugha ya Kiswahili hatuna toni.
Kidatu ni kiwango cha juu, cha kati,au cha chini katika usemaji pia kidatu ni kile kiwango cha sauti kisikikacho yaani katika usemaji mtu anaweza kuongea kwa sauti ya juu yaani kidatu cha juu, kwa sauti ya kati yaani kidatu cha kati, kidatu cha chini yaani sauti ya chini.na mawimbi sauti huwa yanabaki yaleyale.
Hivyo basi
MAREJELEO
http://sw.m.wikipedia.org/wiki/Matumizi ya Lugha.
Massamba na Wenzake (2004), Fonolojia ya Kiswahili Sanifu FOKISA, TUKI: Dar es Salaam.
Mgullu, R.S (1999), Mtaala wa Isimu, Fonetiki na Fonolojia ya Kiswahili, Nairobi: longhorn publishers.
Palome, E (1967), A Handbook of Swahili Language
TUKI, (1990) Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha, TUKI: Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni